TANGAZO TIGO

TANGAZO TIGO

Tuesday, September 27, 2016

Je, Madrid kufuta rekodi mbovu Ujerumani mbele ya Dortmund leo?

Real Madrid leo wana kibarua kigumu ugenini nchini Ujerumani kucheza na Borussia Dortmund kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kundi F wa UEFA Champions League utakaochezwa kwenye Uwanja wa Signal Iduna Park.
Wakati Real Madrid wametoka kuvutwa na shati kwenye La Liga kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Las Palmas wikiendi iliyopita, Borussia Dortmund kwa upande wao walikuwa na furaha baada ya kuwafunga Freiburg 3-1.
*Borussia wakiwa katika kiwango bora mpaka sasa wameshinda michezo yao yote minne iliyopita katika michuano yote, wakiwa wamefunga magoli 20. Madrid, kwa upande wa wamekosa njaa ya magoli katika safu yao ya ushambuliaji na kushuhudia wakipoteza pointi katika michezo kadhaa iliyopita.
Lakini kocha wa Madrid Zinedine Zidane, ambaye alishinda kila kitu akiwa mchezaji, anaweza kufanya mabadiliko machache kuelekea mchezo huu katika dimba la Sigbal Iduna Park, sehemu ambayo timu imekuwa na historia mbovu kabisa
Kimsingi kwenye mechi zao za mwisho katika uwanja huo kwenye misimu ya 2012, 2013 na 2014, Real hawajashinda mchezo wowote zaidi ya kuambulia vipigo vitatu na sare moja.
Michezo ya hivi karibuni imewapa Madrid matokea ambayo hawakuwa wametarajia. Kiungo mkabaji Casemiro amethibitisha umuhimu wake kwenye timu hiyo na kukosekana kwake katika michezo kadhaa ukiwepo hu wa leo ni pigo kubwa kwa Real kutokana na kukosa muhimili muhimu katika eneo la kiungo mkabaji.
Kutokuwa katika kiwango bora mchezaji Cristiano Ronaldo ni changamoto kubwa kwa ‘BBC’, na hata katika mchezo dhidi ya Las Palmas alitolewa nje kutokana na kushindwa kucheza vyema.
Luka Modric na Toni Kroos watakuwa na kibarua kizito kuhakikisha wanacheza vyema eneo la kiungo, na kuondoa mapungufu yaliyoonekana kwenye baadhi ya michezo iliyopita hasa eneo la kiungo mkabaji ambalo linamkosa Casemiro.
Vilevile, ni vigumu sana kwa James Rodriguez au Isco kupata nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa leo kutokana aina ya mchezo wa Dortmund. Dortmund chini ya kocha wao Thomas Tuchel wanacheza soka la kasi ambalo litahitaji umakini mkubwa kwa Madrid katika kuzuia mashambulizi.
Dortmund wanajivunia uwepo wan straika wao aliye kwenye kiwango bora Pierre-Emerick Aubameyang bila kusahau Shinji Kagawa na Mario Gotze ambao lwa pamoja wote watauwasha moto kuhakikisha Dortmund wanapata matokeo.
Wengine ni Ousmane Dembele na Emre Mor ambao pia ni msaada mkubwa kwa wakali hao wa Signal Iduna Park.
Madri wanapaswa kuwa makini zaidi ukizingatia kwamba mpaka sasa Dortmund ndio timu yenye magoli mengi zaidi kwenye Bundesliga, wakiwazidi hata Bayern. Hii inaonesha namna gani walivyokuwa na safu hatari ya ushambuliaji.
Head-to-head statistics 
  • Katika jumla ya michezo yote 10 waliyokutana na Dortmund, Real Madrid wameshinda mara 4, sare mara 3 na wamefungwa mara 3.
  • Katika michezo mitano waliyokutana na Real Madrid Signal Iduna Park, Dortmund hawajafungwa hata mchezo mmoja kati ya mitano, wameshinda mara 3 na kutoka sare mara 2.
  • Mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni kwenye robo fainali ya Champions League msimu wa 2013/14. Real walishinda kwa wastani wa mabao 3-2 margin. Mchezo wa kwanza Dortmund walifungwa mabao 3-0 na wao kulipiza nyumbani kwa kushinda mabao 2-0.
  • Real Madrid hawana rekodi nzuri kwa timu za Ujermani wakiwa ugenini kufuatia kufungwa magoli 2-0 na Wolfsburg kwenye robo fainali ya Champions League msimu uliopita. Hata hivyo Real walifuzu baada ya kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano.
CHANZO SHAFFIH DAUDA

Ushindi wa Simba vs Majimaji, Manara atangaza kaulimbiu ya Simba kuelekea October 1







Waswahili husema kipato huleta majivuno, ushindi wa 4-0 ilioupata Simba dhidi ya Majimaji FC, umemfanya msemaji wa klabu hiyo Haji Manara atangaze kauli mbiu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ kwa msimu huu.

 Manara amesema msimu huu Simba haidharau timu timu yeyote kwenye ligi huku akisisitiza timu yake imejipanga kuongoza ligi kudumu hadi mwisho. “Macho yetu na masikio yetu tunaelekeza October 1, ni mechi ya kawaida kama mechi nyingine ya ligi na hatuipi u-special wowote ule. U-special wake ni kwasababu ya kucharuana kwa mashabiki lakini uzito ni ulele tulioutoa kwenye mechi ya Majimaji ndio tutautoa.

 ligi nzima hatutadharau timu yeyote”, amesema Manara mara baada ya mechi kati ya Simba dhidi ya Majimaji. “Tutacheza na Yanga kama tunacheza na mkubwa mwenzetu, hatujali hii ni timu ndogo au kubwa tunatakiwa tuongoze ligi kwa kudumu hadi ligi inamalizika.” “Hatutadharau mechi inayokuja, mechi ya leo ni sawa na mechi inayokuja bila kujali ni Yanga au timu nyingine yeyeyote, kila mechi ni fainali hiyo ndiyo kaulimbiu ya Simba msimu huu.”

CHANZO SHAFFIH DAUDA

Thursday, September 22, 2016

Real Madrid wameshindwa kuvunja rekodi ya Barca La Liga

1Real Madrid wameshindwa kuvunja rekodi ya iliyowekwa na Barca kwenye La Liga ya kushinda mechi 17 mfululizo baada ya kulazimishwa sare na Villarreal katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Haruna Shamte: Sasa tuko vizuri, naweza kucheza popote katika beki ya City

????????????????????????????????????


MLINZI wa Mbeya City FC, Haruna Shamte ‘Chuma Chakavu’ anaamini kuwa msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania Bara ni mgumu ‘kuliko’ lakini kama timu wanataraji kuwa na msimu wa kupenda tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

Ratiba ya raundi ya nne ya Kombe la EFL hadharani, Mourinho vs Guardiola uso kwa uso tena


1


Droo ya raundi ya nne ya Kombe la Ligi nchini England maarufu kama EFL Cup imefanyika Usiku wa kuamkia leo ambapo timu mbalimbali zimesgajua wapinzani wao.

Barcelona yapata pigo, kumkosa Messi wiki tatu

Staa wa Barcelona Lionel Messi atakuwa nje kwa muda wa wiki tatu baada ya kupata maumivu ya nyonga kwenye mchezo dhidi ya Atletico Madrid uliochezwa Nou Camp na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 jana.
Nohodha huyo wa Argentina alipata maumivu hayo punde tu baada ya kumaliza kuwania mpira na beki wa Atletico Madrid Diego Godin na kuanza kuashiria hali ya maumivu hasa kwenye upande wake wa kulia.Jeraha hilo la Messi inaelezwa awali alipata wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina wiki chache zilizopita, na staa huyo anatarajiwa kuukosa mchezo wa Champions League dhidi ya Borussia Monchengladbach.
Messi pia atakosa michezo La Liga dhidi ya timu za Sporting Gijon na Celta Vigo, na atakuwa hatihati pia kucheza mchezo wa Champions League dhidi ya Manchester City utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.
“Kumkosa Messi maana yake ni pigo katika soka. Tunapokuwa na Messi maana yake tuko imara, lakini tutajitahidi kuwa imara hata bila ya uwepo wake,” kocha wa Barcelona Luis Enrique aliwaambia waandishi baada ya mchezo.

Wednesday, September 21, 2016

SAMATTA NA GENK KATIKA WAKATI MGUMU KIDOGO KAMA MAN UNITED

KRC Genk Jumapili imefungwa mechi ya tatu mfululizo baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Anderlecht Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji
.
Mabao yaliyoizamisha Genk katika mchezo huo ambao Nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta hakucheza kabisa yalifungwa na beki Msenegali Serigne Modou Kara Mbodji dakika ya 64 na mshambuliaji Mtunisia, Hamdi Harbaoui dakika ya 76. 
Genk walipoteza mchezo huo wakitoka kuanza vibaya hatua ya makundi ya Europa League baada ya kufungwa mabao 3-2 na wenyeji Rapid Viena katika mchezo wa Kundi F Alhamisi iliyopita Uwanja wa Allianz, Viena, Austria

.
Na akina Samatta waliingia kwenye mchezo na Rapid Viena wakitoka kufungwa 2-0 na Standard Liege katika Ligi ya Ubelgiji pia. Mara ya mwisho Genk kushinda ilikuwa ni Agosti 28, 2016 waliposhinda 1-0 dhidi ya Zulte-Waregem, bao pekee la kiungo wa Hispania, Alejandro Pozuelo Melero dakika ya 80.
Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita

.
Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 11 alitokea benchi nane msimu uliopita na tatu msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.

Genk watakuwa na mechi mbili mfululizo ugenini, kuanzia leo Uwanja wa Complex Bredestraat mjini Linter dhidi ya Eendracht Aalst Kombe la Ubelgiji na Jumapili dhidi ya Kortrijk Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk katika Ligi ya Ubelgiji, kabla ya Alhamisi wiki ijayo kurejea kwenye Europa League watakapoikaribisha Sassuolo ya Italia katika mchezo wa pili wa Kundi F.

Geita Gold Sport yakubali matokeo FDL yalipangwa, soma hapa ilivyokuwa…


JANA nilikuwa nikifuatilia kipindi cha Michezo Times FM ‘Doko-doko’ mwenyekiti wa Geita, Seif Kulunge amekiri kuwa sauti iliyowahi kusambaa katika mitandao ya kijamii ikihusisha baadhi ya viongozi wa Geita Sport na wale wa TFF ni sauti alisi ya kile kilichotakiwa kutendeka.
Amezungumza mengi, ikiwemo la rais wa TFF, Jamal Malinzi kujikopesha zaidi ya Tsh.150 milioni kutoka katika udhamini wa Kilimanjaro.
“Kile kikao (cha upangaji wa matokeo-sauti yake iliwahi kusambaa katika mitandao ya kijamii) kiliitishwa na wahusika wenyewe (baadhi ya watendaji wa TFF) baada ya kuona kwamba plan A imekataa (Geita Sport walikataa kupanga matokeo).
“Kwa hiyo plan B walitakiwa watuite pale ili watueleze kwamba bila milioni 25 ile ‘ngoma itakataa’ na hela zenyewe zilifanyika katika mgawanyo maalumu ulikuwa unaeleweka. Ni nani apewe shilingi ngapi, nani apewe nini.”
“Kwa kweli hicho ni kitu ambacho kinajulikana na watu wenyewe wanafaham kwamba nani na nani walitakiwa wapewe. Kwa hiyo, kwa nafasi fulani sipendi sana kulizungumzia hilo kwa sababu tunataka kuchunguza zaidi pale tutakapopata ripoti ya TAKUKURU.” anasema, Kulunge mwenyekiti wa Geita Gold Sport.
“Moja ya vitu ambavyo vinatakiwa vitolewe taarifa ni hilo. Kwa hiyo kama ni hivyo TAKUKURU wenyewe wanajua, hivyo nikianza kusema mengi hapa nitakuwa navuruga ripoti ya TAKUKURU kiasi ambapo itakapokuja itakinzana.”
“Tuiachie Serikali kwa nafasi yake na muda wake tuone watatuambiaje ili tuamini kwamba hiki kilichokuwa kinasewa ni cha kweli au. Kama kitakuwa ni cha uongo sisi tupo tayari kutoa (ripoti), lakini tutatoa katika nafasi gani, tutajua sisi. Kama ni kwenda ‘kuhiji’ Chato au tunaenda wapi, lakhni tutaitoa.”
“Na leo namwambia Mh. Nape (Waziri wa habari na michezo,) tukishindwa kuyapata hayo kwenye ripoti zake kwa kweli tunaenda kuhiji Chato. Sisi wana Geita tutaenda kuhiji Chato. Wenzetu wanaenda kuhiji Macca, wanaenda Israel, sisi tutaenda kuhiji Chato mpaka kieleweke.” anaongeza kusema, Kulunge.
Kuhusu jina la Jamal Malinzi kuhusika katika kikao cha upangaji matokeo
“Ukweli halisi wa kuhusika kwa jina la Jamal Malinzi katika sauti ile, hatuwezi kufanya kitu bila kuwa na Jamal Malinzi. Timu ile (Geita Gold Sport) baada ya kupata mdhamini, Malinzi alikuwa yuko karibu sana na hiyo timu katika mazingira yote. Na upo uwezekano wa kutumia jina lake ama ikawa ni kweli kwa sababu hata sisi navyokwambia, mpaka yule kocha  wa timu yetu  (Suleimani Matola) aliletwa na Jamal Malinzi.”
“Sisi kocha tuliyemtaka ni Minziro (Fred Felix) ambaye alitakiwa kuja pale, lakini baada ya kuona kwa heshima na taadhima tukamchukua Matola kwa msaada wa Malinzi.” anasema mwenyekiti huyo wa Geita ambayo imeshushwa hadi ligi daraja la Pili.

CHANZO SHAFFIH DAUDA

Kilimanjaro Queens bingwa CECAFA wanawake

Timu ya taifa ya soka la wanawake Tanzania bara, ‘Kilimanjaro Queens’ imefanikiwa kutwaa ubingwa wa baraza vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kuifunga Kenya kwa magoli 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa mjini Jinja nchini Uganda.
Mkongwe Mwanahamisi Omari aliifungia Kilimanjaro Queens bao la kuongoza dakika ya 26 kabla ya Stumai Abdalla kuzama nyavuni dakika ya 44 kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Christine Nafula aliifungia Kenya goli pekee dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kwenye mchezo huo wa fainali.
Safari ya Kilimanjaro Queens ilianza Septemba 9 ikiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma walikabidhiwa bendera ya taifa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tayari kuelekea Jinja nchini Uganda baada ya kuhitimisha kambi ya siku chache mjini Bukoba.
Kabla ya kuelekea Jinja, Kilimanjaro ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.
Wanadada hao wa Tanzania bara waliwasili Uganda wakiwa tayari kukipiga kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania iliangukia kwenye Kundi B kundi lililokuwa na timu tatu (Tanzania, Rwanda na Ethiopia).
Ilianza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Rwanda kisha ikatoka suluhu na Ethiopia na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa matokeo ya kurushwa shilingi kufuatia kulingana pointi na Ethiopia.
Kwenye husu fainali wakakutana na wenyeji wa mashindano hayo timu ya Uganga ambapo Kilimanjaro ikafuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Uganda kabla ya kuishindaKenyanakutangazwa mabingwa wa CECAFA ya wanawake.

 CHANZO SHAFFIH DAUDA

MINO RAIOLA ARUSHA KIJEMBE KWA ARSENAL JUU YA POGBA

Wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amezungumzia uhamisho wa mchezaji wake kwenda Manchester United, na kudai kwamba ingekuwa rahisi pia kwenda Real Madrid, lakini akiondoa uwezekano wowote wa mchezaji huyo kwenda Arsenal kwa kusema timu hiyo haina soka la kuweza kuvutia usajili wa mchezaji wa kiwango cha dunia.
Raiola amesisitiza kwamba ni kweli Arsenal wana pesa za kufanya usajili huo na kuonesha heshima yake waziwazi kwa Arsene Wenger, japokuwa anaamini timu hiyo imekosa kujiamini pale linapokuja suala la usajili wa wachezaji.
“Hapa sizungumzii tu suala la matumizi ya pesa,” Raiola ameliambia gazeti la Daily Mail. “Ni suala la kufanya maamuzi na kusema ‘ndio huyu ni mchezaji wangu’. Arsenal wana pesa, lakini wana mpira wa kuvutia wachezaji?
“Namheshimu sana Arsene Wenger. Ana falsafa ambazo anapenda kuzitumia ambapo hupenda kusema kiasi ninacholipa hakiendani na thamani ya mchezaji, lakini sio mbaya hakuna shida. Najua vizuri kwamba Wenger anampenda Pogba lakini bei ambayo Juventus waliiweka kumuuza mchezaji huyo haiendani na falsafa zake.
“Kwa upande wa Real Madrid, Zidane alikuwa tayari kwa kila kitu lakini hatukuwa na uhakika kama klabu yake ilikuwa ina mtazamo kama wake. Manchester United walitutumia message na kusema: ‘hii ni klabu kubwa duniani, hakuna tunachoweza kushindwa’.

”CHANZO SHAFFI DAUDA

SERENGETI BOYS IMEWATENDEA HAKI WATANZANIA – NNAUYE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye amesema Serengeti Boys imewatendea haki watanzania kwa kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Congo Brazzaville.
“Vijana wamewatendea haki watanzania, tulijaa uwanjani kuwashangilia wamefanya kazi nzuri sana. Timu waliyopambana nayo ni timu nzuri lakini kwa matokeo waliyoyapata ni kutokana na kazi nzuri, mimi nawashukuru nawaombea heri kwenye mchezo unaofuata tunaamini watafanya vizuri”, alisema Mh. Nnauye mara baada ya mechi kumalizika na Serengeti kuibuka na ushindi wa magoli 3-2.
Serengeti inatarajia kucheza mechi yake ya marudiano dhidi ya Brazzaville baada ya wiki mbili huku ikiwa na matumaini ya kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo baada ya kushinda mchezo wa kawanza.CHANZO SHAFFII DAUDA

Amis Tambwe anasimama pekee na magoli yake 58 VPL

MSHAMBULIZI wa klabu ya Yanga SC, Mrundi, Amis Tambwe alifunga goli lake la tatu msimu katika ushindi wa Mwadui FC 0-2 Yanga.
Tambwe ameshatwaa mara mbili tuzo ya ufungaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara katika misimu mitatu iliyopita alianza kufungua akaunti yake ya magoli wiki iliyopita alipofunga mara mbili katika ushindi wa Yanga 3-0 Majimaji FC hadi sasa amefikisha jumla ya magoli 58 katika ligi kuu pekee.
Alifunga jumla ya magoli 19 katika msimu wake wa kwanza ambao alishinda tuzo ya ufungaji bora akiwa na kikosi cha Simba SC msimu wa 2013/14.
Msimu wake wa pili alianza kwa kufunga katika sare ya Simba 2-2 Coastal Union mwezi Septemba 2014, lakini hadi anajiunga na Yanga kama mchezaji huru mwishoni mwa mwezi Desemba 2014 mshambulizi huyo hakuwa amefunga goli lolote.
Mambo yalianza kumnyookea tena kwani alifanikiwa kufunga jumla ya magoli 14 akiwa Yanga na kufikisha magoli 15 kufikia mwisho wa msimu wa 2014/15.
Msimu wake wa pili alimaliza katika nafasi ya pili ya ufungaji nyuma ya mchezaji mwenzake wa Yanga, Saimon Msuva ambaye alishinda tuzo hiyo baada ya kufunga magoli 17. Msimu uliopita (2015/16,) Tambwe alishinda kwa mara ya pili tuzo ya ufungaji bora baada ya kufunga jumla ya magoli 21.
Mrundi huyo ni hatari kwa mipira ya kichwa na amekuwa na shabaha ‘isiyokwisha’ anapopiga shuti golini. Baada ya kusainiwa kwa Mzambia, Obrey Chirwa ilidhaniwa labda utakuwa mwisho wa kutamba kwa Tambwe lakini tayari ameonesha bado ana njaa ile ile tu.
Huyu ni mshambuliaji-mfungaji bora zaidi katika ligi ya Tanzania Bara katika kipindi cha miaka 16 iliyopita. Ni mfungaji ambaye si rahisi kupatikana, ana mwendelezo bora katika ufungaji msimu hadi msimu. Amis Tambwe anasimama pekee na magoli yake 58 VPL CHANZO SHAFII DAUDA