
Droo ya raundi ya nne ya Kombe la Ligi nchini England maarufu kama EFL Cup imefanyika Usiku wa kuamkia leo ambapo timu mbalimbali zimesgajua wapinzani wao.
Katika droo hiyo imeshuhudiwa mahasimu wawili wa jiji la Manchester yaani Manchester na United wakikutana kwenye mchezo utakaofanyika Oktoba 24.
Hii inkuwa mara ya pili kwa United na City kukutana mara baada ya hapo awali kukutana kwenye mchezo wa Premier League ambapo, Man City walishinda mabao 2-1 kwenye mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Old Trafford.
Ratiba ya michezo yote hii hapa
Katika mchezo huo Manchester United kwa mara nyingine tena watakuwa wenyeji dhidi ya mahasimu wao Manchester City.
CHANZO SHAFFIH DAUDA
No comments:
Post a Comment