TANGAZO TIGO

TANGAZO TIGO

Wednesday, September 21, 2016

Geita Gold Sport yakubali matokeo FDL yalipangwa, soma hapa ilivyokuwa…


JANA nilikuwa nikifuatilia kipindi cha Michezo Times FM ‘Doko-doko’ mwenyekiti wa Geita, Seif Kulunge amekiri kuwa sauti iliyowahi kusambaa katika mitandao ya kijamii ikihusisha baadhi ya viongozi wa Geita Sport na wale wa TFF ni sauti alisi ya kile kilichotakiwa kutendeka.
Amezungumza mengi, ikiwemo la rais wa TFF, Jamal Malinzi kujikopesha zaidi ya Tsh.150 milioni kutoka katika udhamini wa Kilimanjaro.
“Kile kikao (cha upangaji wa matokeo-sauti yake iliwahi kusambaa katika mitandao ya kijamii) kiliitishwa na wahusika wenyewe (baadhi ya watendaji wa TFF) baada ya kuona kwamba plan A imekataa (Geita Sport walikataa kupanga matokeo).
“Kwa hiyo plan B walitakiwa watuite pale ili watueleze kwamba bila milioni 25 ile ‘ngoma itakataa’ na hela zenyewe zilifanyika katika mgawanyo maalumu ulikuwa unaeleweka. Ni nani apewe shilingi ngapi, nani apewe nini.”
“Kwa kweli hicho ni kitu ambacho kinajulikana na watu wenyewe wanafaham kwamba nani na nani walitakiwa wapewe. Kwa hiyo, kwa nafasi fulani sipendi sana kulizungumzia hilo kwa sababu tunataka kuchunguza zaidi pale tutakapopata ripoti ya TAKUKURU.” anasema, Kulunge mwenyekiti wa Geita Gold Sport.
“Moja ya vitu ambavyo vinatakiwa vitolewe taarifa ni hilo. Kwa hiyo kama ni hivyo TAKUKURU wenyewe wanajua, hivyo nikianza kusema mengi hapa nitakuwa navuruga ripoti ya TAKUKURU kiasi ambapo itakapokuja itakinzana.”
“Tuiachie Serikali kwa nafasi yake na muda wake tuone watatuambiaje ili tuamini kwamba hiki kilichokuwa kinasewa ni cha kweli au. Kama kitakuwa ni cha uongo sisi tupo tayari kutoa (ripoti), lakini tutatoa katika nafasi gani, tutajua sisi. Kama ni kwenda ‘kuhiji’ Chato au tunaenda wapi, lakhni tutaitoa.”
“Na leo namwambia Mh. Nape (Waziri wa habari na michezo,) tukishindwa kuyapata hayo kwenye ripoti zake kwa kweli tunaenda kuhiji Chato. Sisi wana Geita tutaenda kuhiji Chato. Wenzetu wanaenda kuhiji Macca, wanaenda Israel, sisi tutaenda kuhiji Chato mpaka kieleweke.” anaongeza kusema, Kulunge.
Kuhusu jina la Jamal Malinzi kuhusika katika kikao cha upangaji matokeo
“Ukweli halisi wa kuhusika kwa jina la Jamal Malinzi katika sauti ile, hatuwezi kufanya kitu bila kuwa na Jamal Malinzi. Timu ile (Geita Gold Sport) baada ya kupata mdhamini, Malinzi alikuwa yuko karibu sana na hiyo timu katika mazingira yote. Na upo uwezekano wa kutumia jina lake ama ikawa ni kweli kwa sababu hata sisi navyokwambia, mpaka yule kocha  wa timu yetu  (Suleimani Matola) aliletwa na Jamal Malinzi.”
“Sisi kocha tuliyemtaka ni Minziro (Fred Felix) ambaye alitakiwa kuja pale, lakini baada ya kuona kwa heshima na taadhima tukamchukua Matola kwa msaada wa Malinzi.” anasema mwenyekiti huyo wa Geita ambayo imeshushwa hadi ligi daraja la Pili.

CHANZO SHAFFIH DAUDA

No comments:

Post a Comment