TANGAZO TIGO

TANGAZO TIGO

Wednesday, November 23, 2016

KIVUMBI CHA KOMBE LA TFF KUENDELEA WIKI IJAYO


BAADA Baruti ya Mara kuifunga Ambassador ya Simiyu mabao 3-1 katika mchezo wa Raundi ya pili  ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC), Uwanja wa Halmashauri ya Kahama, michuano hiyo itaendelea Novemba 27, mwaka huu kwenye viwanja mbalimbali kwa mujibu wa ratiba.

Hatua ya pili itakutanisha timu zlizopenya hatua ya kwanza iliyofanyika wikiendi iliyopita. Mechi zinazotarajiwa kucheza hatua inayofuata ni Tomato dhidi ya Jangwani katika mchezo utakaofanyika mkoani Njombe.

Mbuga FC ya Mtwara itacheza na Muheza United huko Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara huku Kabela City ya Kahama itakuwa mwenyeji wa Firestone ya Kiteto mkoani Manyara.


Raundi ya tatu itafanyika Desemba 3, 2016 kwa kukutanisha timu za Mtwivila ambayo itasubiri mshindi kati ya Tomato na Jangwani wakati Stand Bagamoyo itasubiri mshindi kati ya Mbuga na Muheza United ya Tanga huku Stand Misuna inasubiri mshindi wa mchezo kati ya Kabela City na Firestone ya Manyara ilihali Mrusagamba ya Kagera sasa inasubiri kucheza na Baruti ya Mara.

Kufika hapo Tomato iliing’oa Mkali ya Ruvuma kwa ushindi wa penalti 6-5; Jangwani iliifumua Nyundo 2-0; Mtwivila iliilaza Sido kwa mabao 7-4; Mbuga iliifunga Makumbusho mabao 5-4; wakati Muheza ilishinda 2-1 dhidi ya Sifa Politan ya Temeke.

Timu ya Stendi FC ililala kwa Kabela City kwa mabao 5-3; wakati Stand Misuna iliifunga Veyula mabao 2-1 huku Stand ikiilaza Zimamoto mabao 5-4 ilihali Baruti FC ya Mara na Mrusagamba ya Kagera zilipita baada ya wapinzani Gold Sports ya Mwanza na Geita Town kugomea mechi za awali kwa kutojitokeza uwanjani.

POSTED BY MINDI JOSEPH

MALINZI AWAPA POLE YANGA KWA MSIBA WA PILI NDANI YA WIKI MOJA


RAIS wa  Shirikisho la Soka Tanzania  (TFF), Jamal Malinzi amewapa pole mabingwa wa nchi, Yanga SC kufuatia msiba wa pili ndani ya wiki moja, baada ya kifo cha aliyewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu, miaka ya 1990, Hamad Kiluvia.

Hamad Kilivua amefariki dunia leo alfajiri Novemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ambayo Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Isaac Shekiondo ‘Clinton’ amezikwa kwao Korogwe mkoani Tanga.

Malinzi amesema kifo cha Kiluvia kinaongeza majonzi kwa wana Yanga, kwani kinakuja wakati bado machozi ya kumlilia Shekiondo aliyefariki dunia Novemba 20, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana, Ilala  jijini Dar es Salaam hayajaisha.


Enzi za uhai wake, Kiluvia pia aliwai kuwa Mjumbe wa Bodi ya Seneti ya klabu hiyo pamoja na Malinzi, aliyekuwa pia Katibu Mkuu wa timu hiyo ya Jangwani.

Kadhalika Rais Malinzi alituma salamu hizo kwa familia ya marehemu Kiluvia ndugu, jamaa na marafiki ambayo kwa muda walikuwa wakimuuguza mpendwa wao na hivyo kutokana na kifo hicho, amewataka kuwa watulivu kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.
.
Msiba wa Kiluvia uko nyumbani kwake, Mikocheni Regent Estate jirani na Ofisi za Baraza la Mazingira (NEMC) ambako taratibu za mazishi zinafanyika. 

POSTED BY MINDI JOSEPH

ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA PSG EMIRATES


Alexis Sanchez akikimbia kushangilia baada ya kiungo wa PSG, Marco Verratti kujifungia kuipatia bao la pili Arsenal dakika ya 60 lililoelekea kuwa la ushindi kabla ya PSG kusawazisha na 

mchezo huo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Playa kumalizika kea are ya 2-2 Uwanja wa Emirates. Bao lingine la Arsenal lilifungwa na Olivier Giroud dakika ya 45, wakati ya PSG yalifungwa na Edinson Cavani dakika ya 18 na Alex Iwobi dakika ya 77 aliyejifunga pia.

 Kwa matokeo hayo, Arsenal na PSG zote zimesonga mbele kutoka kundi hilo  

POSTED BY MINDI JOSEPH

MESSI AIFUNGIA MABAO YOTE BARCELONA YASHINDA 2-0 SCOTLAND


Muargentina Lionel Messi akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Barcelona mabao yote dakika za 24 na 55 kwa penalti katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji Celtic.

 Uwanja wa Celtic Park mjini Glasgow, Scotland katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya. Barca imesonga mbele pamoja na Manchester City 


POSTED BY MINDI JOSEPH

MAN CITY YACHOMOA UJERUMANI, SARE 2-2 LIGI YA MABINGWA

Kiungo wa Hispania  David Silva (kulia) akiushuhudia mpira alioupiga ukielekea nyavuni dakika ya 45 na  kuipatia Manchester City bao la kusawazisha .

katika sare ya 1-1 na wenyeji, Borussia Monchengladbach Uwanja wa  Borussia-Park mjini Monchengladbach katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bao la wenyeji lilifungwa na Raffael dakika ya 23 .

POSTED BY MINDI JOSEPH

Monday, November 21, 2016

SAMATTA ACHEZA DAKIKA SITA TU GENK YAUA 2-0 UBELGIJI

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 2-0 dhidi ya AS Eupen katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Samatta aliingia uwanjani dakika ya 84 kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis katika mchezo ambao mabao ya Genk yalifungwa na beki wa Mali, Ibrahim Diallo aliyejifunga dakika ya 20 na Alejandro Pozuelo dakika ya 38.

Huo unakuwa mchezo wa 33 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 13 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita
.

Katika mechi hizo, ni 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 15 alitokea benchi nane msimu uliopita na 12 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu
.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Bizot, Nastic, Colley, Brabec, Castagne, Ndidi, Pozuelo, Susic/Heynen dk65, Bailey, Buffalo dk76' Trossard) and Karelis (82 'Samatta).
KAS Eupen: Crombrugge, Diallo, Abdourrahman, Diagne, Lazare/Dufour), Garcia, Bassey, Sylla (80 Taulemesse) Onyekuru, Blondelle (88' Hackenberg) Oncansey

chanzo saleh jembe

SIMBA SC YAKUBALI KUTOA SH MILIONI 240 KUREJESHEWA OKWI

SIMBA SC imekubali kulipa dola za Kimarekani 120,000, zaidi ya Sh. Milioni 240 kwa klabu ya Sonderjiske ya Denmark ili kurejeshewa mshambuliaji wake, Mganda Emmanuel Okwi.
Na baada ya Simba SC kulipa fedha hizo, Okwi atarejea kufanya kazi Msimbazi kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa mujibu wa makubaliano hayo.


Simba SC ilimuuza Okwi kwa dola 100,000 mwaka juzi Denmark, lakini kutokana na mchezaji huyo kutopata nafasi ya kucheza Ulaya, inaamua kumrejesha na makubaliano yamefikiwa.



"Dola 120,000 tu wale jamaa wanataka watuachie Okwi. Na Okwi naye atasaini kwa mshahara tu mkataba wa mwaka huu, hatumpi dau la kusaini yeye,"kimesema chanzo kutoka Simba. 

Okwi ni mchezaji aliyeipa faida kubwa Simba ndani na nje ya Uwanja enzi zake anacheza Msimbazi. Mbali na kuwasaidia Wekundu wa Msimbazi kushinda matajii mbalimbali tangu ajiunge nao kwa mara ya kwanza mwaka 2010, Okwi pia ameinufaisha kifedha Simba SC
.
Simba ilimuuza Okwi Etoile du Sahel ya Tunisia Januari mwaka 2013 kwa dau la rekodi kwa klabu za Tanzania, dola 300,000, ingawa baada ya muda akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo ya Tunisia.

Mtafaruku ulianza baada ya Okwi kuchelewa kurejea mjini Sousse mkoani Sahel baada ya ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa, Uganda.

Okwi naye akadai Etoile walikuwa hawamlipi mishahara na kufungua kesi FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa), ambayo mwisho wa siku alishinda kwa kuruhusiwa kutafuta timu nyingine ya kuchezea kulinda kipaji chake, wakati wa mgogoro wake na klabu ya Tunisia.
Okwi akajiunga na SC Villa ya kwao, Kampala katikati ya mwaka 2013 na Desemba mwaka huo, akahamia Yanga SC.

Hata hivyo, Okwi akavunja Mkataba na Yanga SC Agosti waka 2014, baada ya timu hiyo ya Jangwani kushindwa kumlipa dola za Kimarekani 60,000 kama ilivyokuwa katika Mkataba baina yao na kurejea klabu yake ya zamani, Simba.

Na mapema Oktoba mwaka 2014, Simba SC nayo ilimuuza Okwi  SonderjyskE FC ya Ligi Kuu ya Denmark ambako alisaini Mkataba wa miaka mitano.
Akiwa katika mwaka wa pili wa Mkataba wake wa miaka mitano, Okwi anatarajiwa kurejea Simba tena

chanzo saleh jembe

KOCHA HEMED MOROCCO WA TAIFA STARS ANUKIA STAND UNITED YA SHINYANGA



Baada ya Mfaransa, Patrick Liewig kuachana na Stand United, sasa imeelezwa mikoba yake itachukuliwa na Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco ambaye tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na uongozi wa klabu hiyo.

Morocco ambaye amewahi kuzinoa Coastal Union na Timu ya Taifa ya Zanzibar, ataungana na Athuman Bilal ‘Bilo’ katika kuiongoza timu hiyo inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa katibu wa klabu hiyo, Kennedy Nyangi, ni kwamba, baada ya kuwa na mazungumzo na makocha wengi, lakini wamefikia maamuzi ya kukaa chini na kumalizana na kocha huyo.

“Tulikuwa na mazungumzo na makocha wengi ili kuziba nafasi ya Liewig, kati ya hao tumeona Hemed Morocco anafaa kuwa kocha wetu mkuu, kilichobaki kwa sasa ni kuona ni kwa namna gani tunamalizana naye,” alisema Nyangi


chanzo saleh jembe

Sunday, November 20, 2016

MAHAFALI YA 11 YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA YAFANA JUMAMOSI YA TAREHE 19-11-2016

Sunday, November 20, 2016





Sherehe ya mahafali ya 11 ya chuo cha uandishi na habari na utangazaji Arusha (AJTC) imefanyika mapema jana katika ukumbi wa PPS ikihudhuriwa na wengi  huku mgeni rasmi akiwa ni mea wa jiji la Arusha na diwani wa kata ya Sokoni one Mh  Calist Lazarro.


Sherehe hizo zilianza na maandamano kuelekea ukumbini hapo ambapo shughuli nzima ilifanyika kwa ustadi mkubwa na washereheshaji wakiwa ni Samson Festo na Amosi Thomas Ishengoma ambao walisherehesha mahafali hayo yaliyosubiriwa kwa hamu na walio wengi.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo waliohitimu wahitimu 38,Mh Lazarro licha ya kuwataja waliofanikiwa kupitia chuo hicho pia amewataka wahitimu kupambana na sera zinazoibana tasnia kama sera ya mwandishi anayetambulika lazima awe amesoma degree ili kuifikisha mbali tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.


Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi waliohitimu hapo jana Bwana Underson Bugoma amesema anamshukuru mungu kwa kumjalia kuhitimu masomo yake salama na kuhaidi atakuwa mwandishi makini na kusimamia ukweli na si kinyume na hapo...

Aidha mmoja wa wanafunzi anayesalia chuoni hapo Bi Asha Kabuga ameeleza kusikitishwa na kuhitimu kwa wanafunzi hao lakini ameeleza kuwa pamoja na kuwapenda na kuwazoea wao bado watawahitaji ili kufika mbali zaidi katika tasnia.

Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ni miongoni wa vyuo ambavyo vinatoa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji nchini  na kinashika nafasi ya pili Tanzania kwa mujibu wa NACTE.



posted by MINDI JOSEPH