Sunday, November 20, 2016
Sherehe ya mahafali ya 11 ya chuo cha uandishi na habari na utangazaji Arusha (AJTC) imefanyika mapema jana katika ukumbi wa PPS ikihudhuriwa na wengi huku mgeni rasmi akiwa ni mea wa jiji la Arusha na diwani wa kata ya Sokoni one Mh Calist Lazarro.
Sherehe hizo zilianza na maandamano kuelekea ukumbini hapo ambapo shughuli nzima ilifanyika kwa ustadi mkubwa na washereheshaji wakiwa ni Samson Festo na Amosi Thomas Ishengoma ambao walisherehesha mahafali hayo yaliyosubiriwa kwa hamu na walio wengi.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo waliohitimu wahitimu 38,Mh Lazarro licha ya kuwataja waliofanikiwa kupitia chuo hicho pia amewataka wahitimu kupambana na sera zinazoibana tasnia kama sera ya mwandishi anayetambulika lazima awe amesoma degree ili kuifikisha mbali tasnia ya uandishi wa habari na utangazaji.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi waliohitimu hapo jana Bwana Underson Bugoma amesema anamshukuru mungu kwa kumjalia kuhitimu masomo yake salama na kuhaidi atakuwa mwandishi makini na kusimamia ukweli na si kinyume na hapo...
Aidha mmoja wa wanafunzi anayesalia chuoni hapo Bi Asha Kabuga ameeleza kusikitishwa na kuhitimu kwa wanafunzi hao lakini ameeleza kuwa pamoja na kuwapenda na kuwazoea wao bado watawahitaji ili kufika mbali zaidi katika tasnia.
Chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Arusha ni miongoni wa vyuo ambavyo vinatoa mafunzo bora ya uandishi wa habari na utangazaji nchini na kinashika nafasi ya pili Tanzania kwa mujibu wa NACTE.
No comments:
Post a Comment